Viongozi na wanachama wapatao 78 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Tanga wametangaza kujiondoa katika chama hicho leo Mei 18, 2025.
Viongozi waliotangaza kujitoa Chadema ni pamoja na
- Fatuma Mahine Katibu Bawacha Mkoa
- Abdalah Msembe katibu wazee Mkoa na mjumbe Mkutano mkuu taifa
- Juma Abdalah katibu wa baraza la wazee Kanda na Wilaya Tanga na Mjumbe mkutano mkuu taifa
- Zainab Ashraff Mjumbe kamati ya mafunzo Kanda ya kaskazini
- Mwanamkuu Jumbe Katibu Bawacha Wilaya Tanga
- Juma Abdalah Katibu wazee Wilaya Tanga
- Hashim Mwakalemba Mwenyekiti Bavicha Wilaya Tanga
- Mussa Kasimka Mjumbe Kamati Tendaji Tanga
- Said Ally Mjumbe kamati tendaji Tanga
- Hussein Ally mjumbe kamati tendaji Tanga.