VIONGOZI DINI YA KIISLAM WATAKIWA KUHAMASISHA JAMII UMUHIMU WA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

Na Saulo Stephen – Singida.

Viongozi wa Dini ya Kiislamu kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa wametakiwa kuhamasisha jamii ya Kiislamu Mkoani Singida kuacha tabia ya kupuuza suala la uchaguzi wa Viongozi wa Serikali hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.

Kaulibhiyo imetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassor wakati akizungumza na Viongozi wa dini hiyo juu ya umuhimu wa suala la uchaguzi Mkuu na kuwapa mwamko wa kushiriki katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini.

Amesema, kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya jamii ya Kiislamu mkoani Singida kusema kuwa kitendo cha kupiga kura au kuchagua Kiongozi ni haramu jambo ambalo shekh Issa Nassor anapinga vikali na kuwataka waisilama mkoani Singida kubadilika na kuachana na tabia sanjari na mtazamo huo.

“Niwaagaze Mahimamu wote pamoja na masheikh wa wilaya katika mkoa wetu wa Singida, na hata mimi mwenyewe shekh wa Mkoa, tutumie nyumba za ibada kwa maana ya misikiti yetu tuzungumze na waumini ili waweze kutambua umuhimu wa kupiga kura na kuchagua viongozi,” amesema Shekh Issa Nassor.

Agizo la Sheikh Issa Nassor linalenga kubadili mtazamo wa jamii ya Kiislamu mkoani humo, ili kushiriki matukio muhimu ya kikatiba ndani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *