Mama mzazi wa Star na Rapa nguli wa miaka ya 1990, Notorious B.I.G, Bi Violetta Wallace amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72 alipokuwa amelazwa kwa uangalizi maalum Hospitalini.
Akithibitisha kifo hicho, Mchunguzi Mkuu wa Kaunti ya Monroe, Thomas Yanac amesema Violetta amefariki dunia hii leo Ijumaa Februari 21, 2025 majira ya asubuhi katika mji wa Stroudsburg uliopo Pennsylvania nchini Marekani.
Mwanaye BIG, alikuwa mmoja wa wana Hip-hop mahiri waliowahi kutawala hadi alipouawa katika shambulio la risasi mwaka 1997, akiwa na umri wa miaka 24 ambapo umaarufu wake ungali bado unaishi hadi sasa.

Violetta alizaliwa Nchini Jamaica na akiwa na mumewe George Latore Wallace walihamia Brooklyn, New York na baadaye walimkaribisha duniani mwana wao wa pekee, Christopher.
Baadaye Latore alitengana na familia yake mwaka 1974, hapo Violetta akifanya kazi kama mwalimu wa shule ya awali na kumlea mtoto wake yeye peke yake.