Vugu vugu la mastaa kutoka mamtoni kuingia kwenye skendo ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono inazidi kukuwa kwa kasi na kwa mara nyingine Staa mwingine wa filamu, Vin Diesel ameshtakiwa kwa kosa la ubakaji dhidi ya msaidizi wa zamani Asta Jonasson.

Diesal anadaiwa kutenda kosa hilo katika hoteli ya St. Regis mnamo 2010 wakati uwandaaji wa filamu ya Fast and Furious ya tano (Fast Five).
Mtandao wa Vanity Fair, unabainisha kuwa “Usiku mmoja mnamo Septemba 2010, Jonasson aliombwa kusubiri katika chumba cha Diesel katika hotelini na Dieasl alipofika chumbani kwakwe alimshika mikono rembo huyo na kumvuta kitandani, ila bibiye aliomba asimame kwanza, na ndipo akamponyoka mikononi na kuondoka katika chumba hicho.”