VIKOSI VYA JESHI LA MADAGASCAR VYACHUKUA NCHI

Kanali wa Jeshi la Madagascar, Michael Randrianirina kupitia Redio ya Taifa amethibisha kuwa vikosi vya Kijeshi vimechukua mamlaka kamili ya kuiongoza Nchi hiyo.

Hatua hiyo, inakuja kufuatia Rais wa Andry Rajoelina kukimbilia ughaibuni kufuatia mvutano mkali kati yake na waandamanaji kizazi cha Gen Z waliokuwa wakiungwa mkono na vikosi vya usalama.

Kanali Randrianirina, ambaye aliongoza uasi wa Wanajeshi waliojiunga na Waandamanaji wa Gen Z wanaopinga serikali, amesema hatua zaidi za kuimarusha utawala zitaendelwa huku akiwataka raia kuwa na utulivu.

Ameongeza kuwa, Jeshi litavunja taasisi zote za Serikali isipokuwa Baraza la Wawakilishi, ambalo lilikuwa limepiga kura ya kumng’oa madarakani Rajoelina dakika chache kabla ya tangazo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *