Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Vijiji 1,239 kati ya 12,318 vyasalia kupata umeme

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amezindua matokeo ya utafiti wa athari za upatikanaji wa Nishati Endelevu Tanzania Bara kwa mwaka 2021/2022 ambao umeonesha kuwa asilimia 72 ya kaya zote Tanzania Bara zinaishi katika vijiji na mitaa iliyofikiwa na huduma ya umeme.

Dkt .Biteko amezindua utafiti huo jijini Dodoma ambapo amesema kuwa, lengo kuu la utafiti huo lilikuwa ni kupima upatikanaji wa nishati endelevu na athari ya upatikanaji wake kwa Tanzania Bara.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa, taarifa ya REA ya mwezi Novemba 2023, inaonesha kuwa, jumla ya vijiji vilivyounganishwa na umeme kwa upande wa Tanzania Bara ni 11,079 sawa na 90% ya vijiji vyote 12,318, aidha Vijiji vilivyobaki 1,239 sawa na asilimia 10 vinatarajiwa kuunganishwa na umeme ifikapo Juni 2024.

Pamoja na mafanikio hayo, Dkt. Biteko amesema kuwa, bado kuna changamoto ya kupatikana kwa nishati endelevu hivyo amewahakikishia wananchi kuwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za muda mfupi na za muda wa kati zitakazowezesha kufikia lengo la nishati safi kwa haraka zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *