Vijana wasikate tamaa, kuweni wabunifu

Vijana nchini wametakiwa kutokata tamaa na kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato badala ya kukaa na kusubiri ajira za serikalini au kutoka kwa watu binafsi.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Revocatus Kagunze Agosti 25 mwaka huu akiwa katika uwanja wa CCM Kambarage katika mashindano ya waeendesha baiskeli yaliyohusisha vijana zaidi ya 80 kutoka katika wilaya mbalimbali mkoani Shinyanga.

Mwalimu Kagunze ameongeza kwamba Manispaa ya Shinyanga kwa kutambua mchango wa vijana katika Maendeleo inatarajia kuendesha mafunzo ya ujasiriamali kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kabla ya kuwapatiwa mikopo ya halmashauri.

Kupitia mashindano hayo wananchi waliohudhuria wamepata nafasi ya kupima afya kwa hiyari na uchangiaji damu pamoja na semina kwa wajarisiamali wanaojihusisha na shughuli za uendeshaji wa Baiskeli,Bodaboda na Bajaj mkoani Shinyanga. Katika hatua nyingine kupitia mashindano hayo baadhi ya waendesha baiskeli mkoani Shinyanga wameiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kuwafadhili kwa kuwawezesha kuwa na baiskeli za kisasa hatua itakayowawezesha kushiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *