Vijana wajifunze kwa wenzao waliofanikiwa

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya vijana uliwenguni, vijana wametakiwa kuwa wabunifu kwa kubadilisha mitazamo yao na namna wanavyoyachukulia mambo ikiwa ni pamoja na kukaa pamoja kati ya vijana waliofanikiwa ili kuwasaidia mbinu za mafanikio wale ambao bado hawajafanikiwa.

Hayo yamesemwa na meneja Mkuu wa Jambo Media Nickson George katika kikao kilichokutanisha wadau wa maendeleo na vijana waliofanikiwa lengo likiwa ni kufungua neno la siri la mafaniko kwa vijana kupita kipindi cha Power Fresh kilichorushwa hewani leo kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4.

Naye Afisa Maendelo ya Jamii Halimashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salome Komba ambaye alikuwa mjumbe katika kikao hicho amewataka vijana kuibua mawazo yanayohusu biashara na kutohofia suala la mitaji kwani wamekuwa wakitoa mitaji kwa vijana huku akiainisha mikopo ambayo tayari imeshatolewa kwa vijana. Siku ya vijana duniani huazimishwa kila mwaka tarehe 12 Agosti na iliwekwa na umoja wa mataifa mwaka 2000 lengo likiwa ni kuelekeza umakini katika masuala ya yanayowazunguka vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *