VIJANA SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO YA STADI ZA KAZI, UMUHIMU WA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

Na Saulo Stephen – Singida.

Vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida, wamepatiwa mafunzo mbalimbali ikiwemo Stadi za kazi, maisha pamoja na umuhimu wa kushiriki katika Uchaguzi mkuu wa 2025.

Mafunzo hayo, ni sehemu ya kongamano lililoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Singida, kwa ajili ya kujiandaa na ujio wa mwenge wa Uhuru, likihusisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Mgori na limefanyika katika shule ya Sekondari Mwanamwema Shein, iliyopo tarafa ya Mgori Singida vijijini.

Baadhi ya Vijana kutoka Tarafa ya Mgori wameishukuru Halmashauri ya Wilaya Singida kwa kuandaa kongamano hilo, ambalo wamesema litawasaidia kujifunza mambo mbalimbali hususani suala zima la stadi za kazi na maisha.

Aidha, wameiomba Halmashauri hiyo kuandaa makongamao kama hayo mara kwa mara hata baada ya Mwenge wa Uhuru kupita, ili kuzidi kuwapa elimu zaidi kuhusu stadi za maisha.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida Julai 19, 2025 katika eneo la Sagara, Wilaya humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *