Na Saulo Stephen – Singida.
Vijana mkoani Singida wametakiwa kujihusisha katika shughuli za ujasiriamali, hususan katika Sekta ya Kilimo, na kujifunza njia sahihi za upatikanaji pamoja na matumizi bora ya pembejeo za Kilimo, ili kuwa na uzalishaji wa mazao wenye tija.
Katibu Tawala Msaidizi wa Huduma za Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji amebainisaha hayo wakati akizungumza na makundi ya vijana kutoka Wilaya za Iramba, Ikungi, Mkalama na Singida kwenye mafunzo ya kuwajengea ya uwezo katika sekta ya kilimo.

Ameyataja makundi yaliyoshiriki katika mafunzo hayo kuwa ni Maafisa ugani kutoka katika halimashauri nne za mkoa wa Singida, Wauzaji na wasambazaji wa pembejeo, pamoja na Wakulima viongozi kutoka katika wilaya hizo nne.

Aidha, Choaji ameongeza kuwa matarajio ni kuwa mafuzo hayo yataongeza ujuzi kwa vijana hao katika kueneza elimu kwa wakulima wa mkoa wa Singida na kuifanya sekta hiyo kuendelea kukua zaidi kwani ndio uti wa mgongo katika uchumi wa mkoa huo.


