VIJANA 160 WAAHIDI UZALENDO WAKIANZA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA BABATI

Jumla ya Vijana 160 Wilayani Babati Mkoani Manyara, wameanza mafunzo ya Jeshi la Akiba, ambapo watajifunza Ulinzi wa Taifa, Ujasiriamali na Stadi mbalimbali.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkuu wa Wilaya Babati, Remidius Mwema amewataka Vijana hao kuwa wazalendo na kutunza mazingira wakati na baada ya mafunzo, ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Awali, akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Babati, Victor King’unza amesema, lengo ni kuwafundisha Ulinzi huo wa Taifa, ujasiriamali na stadi mbalimbali, ili wawe Vijana wema katika jamii.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, wameelezea matarajio yao kuhusu yatakavyo wasaidia na kuwa Wazalenzo pamoja na utunzaji wa Mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *