Idadi ya waliofariki katika Maporomoko ya ardhi mji mdogo wa Katesh, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara imeongezeka na kufikia 80.
Akitoa taarifa hiyo Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Idara ya Habari ya Maelezo, Mobhare Matinyi amesema kati yao 48 ni watu wazima na 32 ni watoto na miili 79 imetambuliwa na ndugu zao huku mmoja ikiwa bado hajatambuliwa.
Amesema mpaka sasa majeruhi ni 133 na kambi za waathirika zipo tatu na majeruhi wanapatiwa matibabu kwa gharama za Serikali.