Tathmini ya Serikali inaonesha kuwa vifo vya watoto vimepungua kwa 35%, kutoka vifo 67 kwa watoto 1000 mpaka kufikia vifo 43 kwa watoto 1000.
Takwimu hizo zimetolewa leo Januari 5, 2024 na Msemaji wa Serikali, Mobhare Matinyi alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa uwasilishaji wa taarifa za serikali jijini Dar es Salaam.
Amesema vifo vinavyotokana na uzazi vimepungua kwa 80%, kutoka vifo 556 kwa vizazi 100,000 mpaka kufikia vifo 101 kwa vizazi 100,000, Lengo likiwa ni kuendelea kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Matinyi amesema lengo la Serikali ni kuondoa kabisa vifo vya watoto wachanga vinavyotokana na changamoto ya afya.