Ubongo una umuhimu mkubwa katika mwili wa binadamu na ndio ambao husaidia kufanya mambo mbalimbali, lakini hata hivyo inaelezwa ya kwamba ubongo wa mwanadamu ndio humfanya mwanadamu kuonekana jinsi alivyo.
Wataalamu wa masuala ya Afya wanasema ili mwanadamu aweze kuongeza akili, katika kufikiri na kutenda mambo mbalimbali anatakiwa kula vyakula vifuatavyo:
- Mafuta ya samaki.
Yenyewe ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama sangara na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja. - Mbegu za maboga.
Hizi zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama
karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, huweza kusaidia kuweza kuongeza akili.
3. Pilipili.
Nacho ni chakula muhimu cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa. Hivyo unaweza ukatumia pilipili kali kama vile pilipili kichaa, pilipili mbuzi kwani hizo ni mifano ya pilipili kichaa.
4. Nanasi.
Ulaji wa Nanasi pia ni miongoni mwa matunda ambayo husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongezea uwezo wa kiakili.
- Nyanya.
Nayo ni muhimu kwani ukiila huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
6. Karanga.
Ni kwa aina zote za Karanga kwani zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
- Mayai ya kienyeji.
Mbali na ladha yake kuwa yenye kuburudisha lakini pia yana kirutubisho aina ya Choline ambacho huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo, hivyo ukila mayai ya kienyeji utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini na kuimarisha afya ya ubongo.


