VIDEO:Adai kupigwa na kuteswa na Polisi

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Dodoma mtaa wa National Housing Kata ya Makole, Kalamba Ramadhani amelalamika kuteswa na watu anao wadhania kuwa ni polisi baada ya kumkamata kinguvu na kumfanyia vitendo vya ukatili ikiwemo kupigwa mpaka kujeruhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Kalamba anadai kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 17 mwaka huu majira ya saa 1 usiku nyumbani kwake baada ya kukamatwa na kupewa adhabu alipelekwa Sentro na kuambiwa anatuhumiwa kwa kuvunja duka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *