Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limetoa taarifa ya mwezi mmoja juu ya hali ya ulinzi na usalama mkoani Simiyu na kusema kuwa hali ni shwari mkoani humo, ingawa jumla ya watuhumiwa 102 wamekamatwa na jeshi hilo kutokana na kujihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu na kwamba kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoni humo ACP. Edith Swebe ameeleza kuwa watu wanane wamefariki dunia kwa kutumbukia kwenye madimbwi ya maji na mito katika kipindi hicho cha mwezi mmoja kwenye maeneo mbalimbali mkoani Simiyu kutokana na mvua zinazoendelea kunyeshakatika kipindi hiki cha masika, ambapo amewaasa wananchi mkoani Simiyu kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua.