VIDEO: Watoto 1,678 wapata mimba ndani ya mwaka mmoja

Licha ya jitihada zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii, bado tatizo la ndoa na mimba za utotoni limeendelea kuwatesa watoto wa kike katika wilaya ya bariadi mkoani Simiyu ambapo jumla ya watoto 1,678 wamekumbwa na tatizo hilo katika kipindi cha mwaka mmoja.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga
wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wilayani Bariadi na kuiasa jamii kubadilika na kuachana na vitendo hivyo ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo katika jamii.

Awali akiwasilisha taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kipindi cha mwaka mmoja, afisa ustawi wa jamii wa wilaya ya bariadi, Janet Jackson ameyataja matendo ya kikatili ambayo yameripotiwa kujitokeza wilayani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *