Idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa kipindupindu imezidi kuongezeka jijini Mwanza ambapo mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 70 wamebainika kuwa na ugonjwa huo.
Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa ambapo amesema ndani ya mkoa huo kumekuwa na ongezeko la kasi la watu wanaougua ugonjwa wa kipindupindu na wanaendelea kupatiwa matibabu katika vituo mbalimbali vya afya vilivyopo ndani ya mkoa huo.