VIDEO: Ukosefu wa elimu chanzo cha wavuvi kushindwa kutumia vizimba

Siku kadhaa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kufanya uzinduzi wa vizimba vya samaki kwa wavuvi wa kanda ya Ziwa, baadhi ya wavuvi kutoka mwalo wa Butuja uliopo ndani ya jiji la Mwanza wameiomba serikali iweze kutoa elimu juu ya matumizi ya vizimba hivyo kwani wengi wao mpaka sasa hawana elimu juu ya matumizi yake.

Wakizungumza na Jambo FM, baadhi ya wavuvi hao wamesema kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na upungufu wa samaki ndani ya Ziwa Victoria na tayari wameona serikali imeanzisha mpango wa kukabiliana na suala hilo kupitia ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba hivyo .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *