VIDEO: Uking’atwa na mbwa nenda kwa daktari wa binadamu siyo wa mifugo

Kila tarehe 28 mwezi Septemba ni siku ya kichaa cha mbwa duniani siku ambayo shirika la umoja wa mataifa la afya ulimwenguni, WHO linaitumia kuelimisha umma juu ya madhara ya ugonjwa huo ambao licha ya kuwa na kinga bado unasababisha vifo hususan barani afrika na asia.

Kwa mkoa wa Shinyanga wananchi wametakiwa kuwa walinzi wa karibu wa mifugo yao vilevile kuwapatia chanjo mbwa kwa wakati ili kujikinga na janga la kichaa cha mbwa kwa wanyama wengine pamoja na binadamu.

Mtaalamu wa mifugo mkoa wa Shinyanga Veran Eugen Mwaluko ametoa wito huo wakati akizungumza na Jambo Fm na kuwasihi wamiliki wa mbwa kuwaepusha mbwa hao na wanyama pori ambao kwa namna nyingine wanaweza kuwa na kichaa ambacho kinaweza kumuathiri mnyama huyo na kuwa hatari pia kwa maisha ya binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *