VIDEO: Saba wakamatwa mauaji wa walinzi

Moja ya Matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakijirudia kila mara katika Mkoa Wa Geita ni maujai ya walinzi wa Makampuni binafsi yanayojihusisha na shughuli za ulinzi.

Imeelezwa kuwa sababu kubwa ya mauji hayo ni kampuni za ulinzi kuajiri walinzi ambao ni raia wa kigeni na wakishaajiriwa muda mchache wanageuka kuwa wahalifu.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi Safia Jongo wakati akizungumza na Jambo Fm ambapo amesema jeshi hilo kwa limeanzisha mkakati wa kuhakikisha kampuni zote za ulinzi zinaajiri watu waliopitia mafunzo ya jeshi la akiba ili kuzidhibiti matukio hayo.

Kamanda Jongo amesema kufuatia tukio la Mauaji ya walinzi wawili lililotokea usiku wa kuamkia disemba 13, 2023 katika kijiji cha Busanda kata ya Busanda wilaya na Mkoa wa Geita jeshi hilo linawashikilia watu 7 wanaotuhumiwa kuhusika na mauji hayo na linaendelea kuwasaka wahusika wote ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *