Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

VIDEO: DC Simalenga atoa neno kwa TASAF

Wakazi wa Mtaa wa Bupandagila uliopo Kata ya Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa nyumba ya mganga kwenye Zahanati ya Gisadi ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za afya na kuondoka na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Wananchi hao wameyasema hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa kupitia TASAF kwenye halmashauri hiyo ambapo wameeleza adha wanazokabiliana nazo kwa sasa kutokana na ukosefu wa nyumba ya mganga katika Zahanati ya Gisadi.

Mratibu wa TASAF wa halmashauri ya mji wa Bariadi Omary Masumo ameeleza sababu ya kutokukamilika kwa ujenzi huo wa nyumba ya mganga hadi sasa na kusema kuwa inatokanana na tatizo la mfumo.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga akaagiza kuharakishwa kwa utkelezaji wa miradi yote ya TASAF ya Halmashauri ya mji wa Bariadi ili ikamilike kwa wakati uliopangwa.

Katika hatua nyingine Simalenga akaitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Wilayani Bariadi kukagua miradi yote inayotekelezwa kupitia TASAF kwenye halmashauri hiyo ili kujua kama taratibu za manunuzi zimefuatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *