Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa mkoa wa Dodoma hautafumbia macho suala la wanafunzi wanaoendelea kusoma kuchelewa kuripoti shuleni kwani limekuwa likiathiri ufundishaji, ujifunzaji na ukamilishaji wa mada.
Senyamule ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2024 kwenye kikao kazi kazi maalum cha wataalam wa elimu na viongozi.
Aidha, Senyamule amewasihi wazazi kuhakikisha wanawaandaa wanafunzi vizuri kwa kuwapatia vifaa vya shule mapema ili waweze kuanza masomo yao kwa wakati, pia ametumia wasaha huo kuwalelekeza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kutekeleza maelekezo hayo kikamilifu.