Kuelekea muhula mpya wa masomo unaotarajiwa kuanza Januari 8 mwaka huu mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewasisitiza wazazi kuhakikisha watoto wao wanashiriki masomo siku ya kwanza na kuondokana na dhana ya kuwa wakienda shuleni wanafanya usafi wiki nzima.
Senyamule ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Michese na kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika halmashauri ya jiji la Dodoma, kata ya mkonze eneo la michese.
Nao baadhi ya wananchi wameelezea kero zao zinazowasumbua huku suala la ardhi na maji likionekana bado kubwa.