Baada Ya Jambo FM Kutoa habari iliyomuhusu Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Dodoma mtaa wa National Housing Kata ya Makole, Kalamba Ramadhani ambaye amelalamika kuteswa na watu anaowadhania kuwa ni polisi baada ya kumkamata kinguvu na kumfanyia vitendo vya kikatili, Jeshi la Polisi, limesema limeanza kufanyia uchunguzi taarifa za kijana huyo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi ACP David Misime amesema jeshi la polisi limeziona taarifa hizo, ambapo wataalamu wengine wa haki jinai watashirikishwa katika uchunguzi huo ili kuhakikisha haki inatendeka.