Mtoto mmoja Agrey Mchanga mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa mtaa wa Kagera wilaya ya Ukerewe jijini Mwanza amefariki dunia baada ya kuganyagwa na gari wakati akiwa amelala chini ya uvungu wa gari hilo.
Akielezea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea Disemba 18, 2023 katika maeneo ya Nansio Ukerewe ambapo inadaiwa mtoto huyo alikuwa ameacha familia yake na kwenda kuishi mtaani baada ya wazazi wake kutengana na siku ya tukio hilo mtoto huyo alikuwa maeneo ya stendi ambapo wakati akiwa amelala chini ya gari dereva wa gari hilo aliingia na kuanza safari ndipo alipomkanyaga mtoto huyo na kusababisha kifo chake.