VIDEO: Majeruhi wa ajali Mwanza awafunguka kilichotokea

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza limethibitisha kutokea kwa ajali ya gari la abiria lenye namba za usajili T 608 DMP mali ya Kampuni ya Batco ambapo mpaka sasa jeshi hilo linamtafuta dereva wa gari hilo kwa ajili ya mahojiano maalumu.

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa mwanza wilbroad mutafungwa amesema ndani ya gari hilo kulikua na abiria 35 ambapo kati yao watu tisa waliokolewa wakiwa hawana madhara yoyote huku wengine 25 wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya magu.

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wakiongea na Jambo FM wameeleza ilivyotokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *