VIDEO: BIL. 40.3 kukusanywa Shinyanga

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 40.3 katika mwaka wa fedha 2024|2025 bilioni 6.0 kati yake zikiwa ni mapato ya ndani,fedha ambazo zinatarajiwa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato.

Kaimu Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Bw.Michael Makotwe amebainisha hayo wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Manispaa hiyo kwa mwaka 2024|2025 katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilichoketi Januari 25 kwa lengo la kujadili mapitio ya bajeti ya halmashauri na kutoa mchanganuo wa upatikanaji wa fedha hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *