Elpidius Edward (22) mkazi wa mtaa wa Katundu Halmashauri ya mjini wa Geita Mkoani Geita amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu baada ya kukutwa na hatia ya kuharibu mali za kanisa na Mahakama ya hakimu Mkazi Geita.
Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya hakimu Mkazi Geita Johari Kijuwile ambapo wakati akimsomea hukumu hiyo amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo Katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Geita Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani.