VETA SHINYANGA YAONGEZA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Chuo cha VETA Shinyanga, kimeendelea kuimarisha utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana ndani na nje ya nchi, ili kuwawezesha kujiajiri na kuajiriwa, sambamba na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Shinyanga na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake leo Machi 2, 2026 Mkuu wa chuo hicho, Abraham Mbughuni amesema  jitihada zinazofanywa na VETA mkoani Shinyanga  zinaendana na maelekezo ya Serikali, inayotoa kipaumbele kwa elimu ya ufundi stadi, kama nguzo ya ajira na maendeleo.

Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Abraham Mbughuni.

Amesema, VETA ina jukumu la kuratibu na kusimamia mafunzo ya ufundi stadi nchini na kwamba baada ya upanuzi wa miundombinu chuoni hapo uwezo wa kudahili wanafunzi umeongezeka kutoka wanafunzi 400 wa kozi muda murefu hadi wanafunzi 545 kwa mwaka huku kozi za muda mfupizikifikia Zaidi ya wanafunzi 3000 kwa mwaka


Ameongeza  kuwa,  katika kuashiria  uimara wa chuo hicho na   ubora wa mafunzo na kwamba umekuwa  umevutia wanafunzi kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, ikiwemo nchi za Uganda kenya,Sudani ya kusini,Iraq na visiwa vya Comoro  hali inayoongeza fursa za ajira kwa wahitimu.

Mbughuni amesema, chuo hicho kwa sasa kinaendelea kutoa kozi mbalimbali ikiwemo umeme wa majumbani na viwandani,ufundi wa magari na umeme wa magari,uchomeleaji na uundaji vyuma, useramala, Tehama, ushonaji na ubunifu wa mavazi,ufundi bomba,ufundi mitambo na mitambo mizito kozi ambazo zimeboreshwa, ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi ya mkoa wa Shinyanga hususa katika sekta za madini ,ujenzi na biashara.



Aidha, ameainisha kuwa Chuo hicho pia kinatoa  mafunzo ya muda mfupi kwa wanawake, vijana wasio na ajira na vikundi vya ujasiriamali. Zaidi ya washiriki 368 wamenufaika kupitia programu maalumu za uwezeshaji, ambayo yanalenga kuwawezesha washiriki kujitegemea kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Ezron Shadrack.

Mbughuni amebainisha kuwa, VETA Shinyanga imeendelea kuwahudumia mafundi waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi kwa kuwafanyia tathmini na kuwapatia vyeti vinavyotambulika kitaifa, hatua inayowawezesha kushiriki katika zabuni na ajira rasmi.


“Dunia ya sasa inahitaji ujuzi wa vitendo zaidi ya vyeti pekee,kwani ujuzi ni mtaji na ajira na nyezo ya kujitegemea na ni heshima huku akiwataka  vijana wajitokeze kwa wingi kujiunga na VETA Shinyanga wajifunze stadi zitakazowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine,” alisema.


Jambo media, pia imefanya mazungumzo na kijana kutoka Kigoma aliyehitimu shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Ezron Shadrack aliyejiunga na chuo hicho cha VETA Shinyanga akisomea kozi ya mitambo mizito ambaye amesema amejiunga chuoni hapo, ili kupata ujuzi wa ziada na kutanua wigo wa ushindani katika siko la ajira.

Naye Mhitimu wa shahada ya kwanza kozi ya Sociology katika chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye amejiunga na VETA Shinyanga, Upendo Zakaria amesema Dunia ya sasa elimu pasipo ujuzi inakosa thamani, ikiwa ni sababu pekee iliyopelekea kujiunga na chuo hicho.

Upendo Zakaria.

Kupitia uwekezaji wa Serikali, VETA imekuwa ni injini ya kuzalisha ajira na uchumi shindani kwa kutoa mafunzo, yanayolenga shughuli mbalimbali za maendeleo na kumwezesha kijana kujua mstakabali wa maisha yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *