Staa kutoka Tanzania aishie Nchini Marekani Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ametangaza kurejea hivi karibuni kwenye muziki ambao alisimama kwa muda kidogo sababu ya malezi ya Watoto wake wawili.
Vee money ameyasema hayo alipokua akijibu maswali ya mashabiki wake ambao wengi walitamani kumsikia tena kwenye muziki ambapo alijibu kwa kifupi tu ‘I promise Soon ๐๐ฟ’ akimaanisha anaahidi hivi karibuni. Hivyo mashabiki wa Vee Money wakae mkao wa kula.
Mpaka sasa ni miaka minne tangu Vanessa Mdee achie kazi yake ya muziki na miaka hiyo aliachia Never Ever ambayo mpaka sasa inawatazamaji 486k