Beki wa Kushoto wa Kimataifa wa Simba SC, raia wa Burkina Faso Valentin Nouma (24) amefunga ndoa na Disemba 28 akiwa nchini kwao Burkina Faso.
Nouma alijiunga na Simba SC ya Tanzania kwa Mkataba wa miaka mitatu mapema mwezi Julai 2024 akitokea St Eloi Lupopo ya Congo DR.
Valentin mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia kwa msimu wa 2022/2023 alishinda tuzo ya beki bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Burkina Faso wakati huo akiwa AS Douanes.