Na Gideon Gregory, Dodoma.
Kufuatia zoezi la uzinduzi wa sera ya Elimu ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na mitaala iliyoboreshwa lililotarajiwa kuzinduliwa januari 31,2025 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan limesogezwa mbele na badala yake kuzinduliwa Februari Mosi 2025.
Taarifa ya kusogezwa mbele tukio hilo imetolewa leo Januari 30,2025 hapa Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa sababu ni kutokana na dharura iliyoshindwa kuzuilika.
‘Tukio la uzinduzi wa wa sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na mitaala iliyoboreshwa limesogezwa mbele baada ya tarehe 31na baadala yake litafanyika jumamosi ya Februari Mosi, 2025 katika ukumbi wa jakaya kikwete kutokana na dharura zilizoshindwa kuzuilika na bado mgeni rasmi ataendelea kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,” ameeleza Prof. Mkenda.