Uongozi wa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga umeanza ukarabati wa uwanja wake kufuatia barua ya kufungiwa kwa uwanja huo kutoka bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyotumwa Oktoba 3, 2023 kwa timu ya JKT Tanzania iliyokuwa ikitumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani ikieleza kuwa umekosa vigezo vya sheria na kanuni za mpira wa miguu.
Akizungumza wakati wa ukarabati wa uwanja huo Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoani Shinyanga Said Makiligo amesema wameanza ukarabati wa uwanja huo mara baada ya kupokea barua ya kufungiwa ili kukidhi viwango vya sheria na kanuni zilizowekwa na bodi ya ligi kuu nchini na kutoa ufafanuzi mara baada utakapokamilika uwanja huo.