UVCCM SHINYANGA YAUNGA MKONO AZIMIO LA MKUTANO MKUU WA JANUARY 19.

Ikiwa imetimia miaka minne tangu Rais Samia Suluhu Hassan akae madarakani Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga (UVCCM) limetoa Kauli ya kuunga mkono Azimio la mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi (CCM) uliofanyika January 19 mwaka huu la kumchagua Rais Samia aendelee kuwa mgombea pekee wa kiti cha Urais wa chama hicho. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Mkoani wa Shinyanga (UVCCM) Bernad Werema katika baraza maalumu la Umoja huo lililoketi manispaa ya Kahama.


“Umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Shinyanga kupitia kikao cha baraza maalum kwa kauli moja tunaunga mkono azimio la mkutano mkuu maalamu wa Ccm Taifa uliofanyika Januari 19 mwaka huu la kumchagua Dr Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025” Alisema Werema.

Sambamba na hilo Umoja huo Umewapongeza Katibu mkuu wa Ccm Taifa Dr. Emmanuel Nchimbi kwa kuchaguliwa kuwa Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Stephen Wasira kwa kuchaguliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa ccm bara.


“Vilevile tunachukua fursa hii kumpongeza Dr.Emmanuel Nchimbi kwa kuchaguliwa kuwa Mgombea Mwenza wa kiti cha Urais Pamoja na ndugu Stephen Wasira kuwa makamu mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Tanzania bara”. Ameongeza Werema.

Katika hatua nyingine Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga umehaidi kuwaunga mkono wagombea wote watakaoteuliwa na chama cha mapinduzi katika Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha chama cha Mapinduzi kinapata ushindi wa Kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.


“Tunahaidi kuwaunga mkono wagombea wote watakaoteuliwa na Chama ngazi ya udiwani na Ubunge ili kuhakikisha mkoa wa Shinyanga unapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa mwaka 2025” Amesisitiza Werema.


Nao baadhi ya wanachi wa Manispaa ya Kahama wamesema kuwa rais Samia amefanya mambo mengi mazuri na anastahili kuongezewa muda ila wanamkwamisha ni baadhi ya watendaji katika halmashauri.


“Kwa muda wa miaka minne Rais Samia amefanya mambo mengi ila wanaomkwamisha ni baadhi ya watendaji wake wa chini ambao hawazingatii maagizo ya serikali” Alisema Mtabaki Kaseke mkazi wa Maalunga Kahama.

One response to “UVCCM SHINYANGA YAUNGA MKONO AZIMIO LA MKUTANO MKUU WA JANUARY 19.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *