Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na uteuzi wa viongozi mbalimbali, ambapo Lazaro Twange ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchiji (TANESCO) na kabla ya uteuzi huu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa Albert Gasper Msando amehamishwa kutoka Wilaya ya Handeni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo na Japhari Kubecha amehamishwa kutoka Wilaya ya Tanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Dadi Kolimba amehamishwa kutoka Wilaya ya Karatu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga na Lameck Nganga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu ambapo kabla ya
uteuzi huo, Nganga alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Bahati Mfungo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu, ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Tarafa ya Mbuguni, Wilayani Arumeru.
Andrew William Massawe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo (SUA) akichukua nafasi ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye amemaliza muda wake.


