UTEKELEZAJI WA ILANI NI USHAHIDI WA UONGOZI IMARA WA CCM – HAPI

Na Saulo Stephen – Singida.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amesema utekelezaji wa Ilani ya CCM, ni ushahidi wa uongozi imara wa chama hicho na serikali yake na kuwataka Wanachi wilayani Ikungi Mkoani Singida kukichagua chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Hapi ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Ifyamahumbi kata ya Mtunduru, jimbo la Ikungi Magharibi, wilayani Ikungi Mkoani Singida awasili mkoani Singida, ambapo aliwanadi wagombea wa CCM akiwemo Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Ubunge wa Ikungi Magharibi Elibarick Kingu pamoja na Madiwani wanaotokana na Chama hicho.

Amewataka wananchi wa Ikungi na Singida kwa ujumla kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu kwa kuwapigia kura wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya diwani, ubunge na Rais.

Kiongozi huyo wa Jumuia ya Wazazi CCM Taifa anaendelea na ziara yake Mkoani Singida lengo ikiwa ni kuwanadi wagombea wa chama hicho pamoja na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuelekea uchaguzi mkuu wa Octoba 29.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *