UTAWALA WA RAIS TSHISEKEDI NI MBOVU – KABILA

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila amesema mgogoro unaoendelea nchini humo unasababishwa na utawala mbovu wa mrithi wake Rais Félix Tshisekedi.

Kabila ameyasema hayo wkati wa mahojiano yake na Gazeti moja la Afrika Kusini, akisema mgogoro huo, ambao ulianza mwaka 2021 ni wa usalama, kibinadamu, kisiasa, kijamii, kimaadili na sera.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila.

Amesema, “katika ngazi ya kitaifa, sababu kuu ya mgogoro huu ni nia ya wazi ya uongozi wa sasa kuvunja Mkataba wa Jamhuri. Mkataba huu, uliotokana na mazungumzo baina ya Kongo huko Sun City, ulipepekea kupatikana kwa Katiba iliyopitishwa na kura ya maoni kiraia mwaka 2006.” 

Kabila ameongeza kuwa, kuvunjwa kwa Mkataba wa Jamhuri kulidhihirishwa kwanza na ukiukwaji wa makusudi na wa mara kwa mara wa Katiba na sheria za nchi na hivyo kuleta mkanganyiko uliopelekea machafuko hao.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi.

Itakumbykwa kuwa, Rais Tshisekedi, alitangaza hadharani nia yake ya kurekebisha Katiba, ambayo alisema inaleta mkwamo wa kidemokrasia.

Hata hivyo, wadadisi wa mambo wanasema kuendelea kwa utawala mbovu wasasa kunaweza kusababisha mawimbi mapya ya machafuko l na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *