Utachagua Kipi kati ya Kubaki Gerezani au Kwenda Vitani?

Ukraine imeanza kuwaachia wafungwa wa kwanza waliokubali kutumikia jeshi chini ya mpango mpya wa kutoa msamaha kwa walio tayari kupigana vita.
Serikali imesema zaidi wafungwa 3,000 waliomba kujiunga na jeshi tangu kupitishwa kwa sheria inayoidhinishwa kusajiliwa kwao mapema mwezi huu.
Hatua hii inakuja wakati huu ambao Ukraine ikikabiliwa na upungufu wa wanajeshi katika uwanja wa vita, na inaakisi mkakati sawa na wa Urusi, ambako maelfu ya wafungwa wamepelekwa nchini Ukraine kwa ahadi ya msahama tangu kuanza kwa uvamizi wa Moscow Februari 2022.
Hata hivyo mpango huo hauhusishi wafungwa waliokutwa na hatua ya vurugu za kingono, mauaji ya watu wawili au zaidi, rushwa kubwa na maafisa wa zamani wa ngazi ya juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *