Afarah Suleiman, Mbulu – Manyara.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Ismail Ally Ussi ameipongeza Wizara ya Maji, kufuatia upatikanaji wa Maji Safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini.
Ussi ametoa pongezi hizo baada ya kukagua na kuridhishwa na mradi wa Maji Dambia Hydom, uliopo katika kijiji cha Harsha Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wenye thamani ya zaidi ya Bilion 41, fedha ambazo zimetolewa na Serikali.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Meneja wa RUWASA Wilaya Mbulu, Onesmo Mwakasege amesema mradi huo utanufaisha jumla ya Vijiji 21.
Nao baadhi ya Wananchi wa Vijiji hivyo wameonesha furaha yao juu ya mradi huo na kuelezea kumbusho la changamoto walizokuwa wakizipata kabla.


