Usiweke Iphone yako kwenye mchele ni hatari

 Kampuni ya Teknolojia inayojishughulisha na utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya kielektroniki zikiwemo simu za iPhone, Apple Inc. imewatahadharisha watumiaji wa bidhaa zake simu za iPhone, kuacha kuweka simu zao kwenye mchele pale inapotokea wametumbukiza au kumwagia maji simu hizo.



Apple wametoa tahadhari hiyo, kupitia tovuti yao, ambapo wamebainisha kuwa kuweka simu hizo kwenye mchele inaweza kusababisha chembechembe ndogo za nafaka hiyo, kuharibu vifaa hivyo.

Endapo ikitokea vifaa hivyo vimeingiliwa na maji, Kampuni hiyo imewashauri wateja wake kuchomoa waya kwenye kiunganishi (port), baada ya hapo uelekeze chini kiunganishi hicho, kisha uiweke katika sehemu kavu yenye hewa safi ikauke.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *