Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Ruth Massam amewataka wasichana na wanawake kufanyakazi kwa bidi, uadilifu, kufahamu unataka nini, kujitambua, kujithamini na kuacha kujichukulia kawaida.
Chanuo msimu wa pili umepiga hodi katika mahakama hiyo na kuzungumza na Jaji ambaye ni mwanamke pekee kwa nafasi hiyo katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
Amesema, tangu akiwa na miaka tisa ndoto zake zilikuwa nikuwa mwanasheria na hakuwahi kuitoa ndoto hiyo katika akili yake.
Katika nafasi za uongozi Jaji Ruth amesema alimaliza chuo mwaka 2001 na 2002 alipata kazi na mekuwa katika nafasi mbalimbali alinaza na nafasi ya Hakimu wa Wilaya Mfawidhi, Hakimu wa Mkoa Mfawidhi, Msajili wa Mahakama Kuu katika Kanda tatu na sasa ni Jaji.
“Mpaka nimefika hapa ubunifu mkubwa katika kufikia nafasi hizi ni kuwa msikivu kwa wale waliokutangulia na kingine ni uajibikaji unapokuwa mama kama hufanyikazi zako kwa uwajibikaji lazima uanguke kwa hiyo vitu hivi viwili ni ngao kubwa siwezi kusema kuna kitu kikubwa nimekifanya.”

Ameongeza kuwa katika safari ya mafanikio ya mwanamke inawezekana kufanya kitu kikubwa ukawa kiongozi kwenye nafasi kubwa kwa kusimama mwenyewe mwanamke bila kumtegemea mwanaume.
Jaji Ruth amesema nafasi kubwa aliyonayo haimuondolei nafasi yake kwa kujihusisha na mambo ya kijamii kutokana na kwamba ametoka kwenye familia na ana ndugu,jamaa na marafiki.
Ameongeza kuwa siku aliyopata nafasi hiyo ya uteuzi kutoka kwa Rais dokta Samia Suluhu Hassan kuwa Jaji alimshukuru Mungu kwa kumfikishaa htua hiyo na kujivunia juhudi katika kazi ambazo zimeonekna na kumuona nafaa katika nafasi hiyo.
Zaidi amewaasa wanasheria wanawake wasikatishwe tamaa na kujiwekea malengo kuungana pamoja na kushikana mikono ili kufika safari yenye mafanikio licha ya kuwepo kwa kundi kubwa la watu wanaokatisha tamaa wenzao.