USHIRIKA NI NJIA PEKEE YA KUWAINUA WAKULIMA KIUCHUMI – RC MACHA

Serikali Mkoani Shinyanga, imesema Ushirika ndio mahala pekee panapoweza kumuinua Mkulima Kiuchumi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha katika jukwaa la ushirika mkoa wa Shinyanga lilofanyika leo Manispaa ya Kahama.

Macha amesema kuwa kupitia misingi ya Ushirika mkulima ananufaika kwa vingi ikiwemo kupata pembejeo kwa urahisi kupitia vyama vya msingi.

Katika hatua nyingine Macha ameomba kukutana na vyama vya ushirika vya Wafugaji,Wachimbaji na watu wa akiba na Mikopo (Saccos) ili kufanya kikao kitakachojadli mikakati ya kuvifanya viwe imara.

Katika hatua nyingine  Macha amekipongeza chama kikuu cha Ushirika (KACU) kwa kuendelea kuwa mfano bora wa ushirika kwa kusimamia vyema misingi ya Ushirika.

Kwa upande wake Mrajis Msaidizi mkoa wa Shinyanya Ibrahim Kakozi amesisitiza matumizi ya tehama na kuwataka viongozi wa vyama vya ushirika kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kukuza uchumi.

 Awali akifungua Jukwaa hilo Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa  Shinyanga Emmanuel Nyambi amesema kuwa lengo la Jukwaa hilo ni Kuambizana mambo yaliyofanywa na Ushirika, Kujadili Changamoto za Ushirika pamoja na kuzitafutia suluhisho lake.

Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Shinyanga 2025 limebebwa na kauli mbiu isemayo Ushirika hujenga ulimwengu ulio bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *