USHINDI WA YANGA DHIDI YA DODOMA JIJI WAMUIBUA MSEMAJI WA SIMBA….

Baada ya ushindi wa Goli 4 – 0 ambazo Yanga ilishinda dhidi ya Dodoma JIJI, Msemaji wa Klabu ya Simba Sports Club, Ahmed Ally ameibuka na kuilalamikia Dodoma JIJI kwa kushindwa kulalamikia matokeo kwa madai aliyosema kuna magoli hayakua ya halali.

Ahmed Ally ameandika ‘Dodoma Jiji jana kafungwa magoli mawili ya Uwongo, Moja la Offside na pili Penati ya ongo lakini Kocha wao hajalalamika kuonewa wala kudhulumiwa zaidi amesema AMESTAHILI KUFUNGWA. – Ahmed Ally.

‘Rejea mechi ya Dodoma Jiji Vs Simba, baada ya sisi kufunga goli la Penati ya halali alitoa mapovu kulaumu Waamuzi yote ni kuaminisha watu kuwa tumemdhulumu na kutaka kutia dosari kazi nzuri inayofanywa na Simba Sports msimu huu’. – Ahmed Ally.

‘Nimeyasema haya ili Wana Simba tuone vita ni kubwa iliyombele yetu ni namna gani Wapinzani hawapendi kufungwa na sisi lakini wanafurahi kufungwa na wengine, ndio maana haishangazi kuona tunapata ushindi wa jasho na damu’. – Ahmed Ally

‘Wale wanaosema tunashinda lakini tunashikilia roho sio kwa sababu tuu ya ubora ni kwa sababu wapinzani wanauma meno kupitiliza na sisi ndio tunapenda ushindani wa aina hiyo Kuelekea mechi zijazo Wana Simba tunapaswa kuunganisha nguvu kweli kweli, tupambane kwa nguvu sawa kuhakikisha tunatimiza malengo yetu’ – Ahmed Ally

Nguvu Moja I Ubaya Ubwela

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *