Ushetu Wahakikishiwa Kupata Maji Ya Ziwa Victoria

Na William Bundala,Kahama

Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amewahakikishia wananchi wa Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kuwa imetenga kiasi shilingi bilioni 44 kwaajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji ya Ziwa Victoria na mchakato wote wa fedha umekamilika na kueleza kuwa mradi huo hautachuka muda mrefu kukamilika.

Waziri Nchemba ameyasema hayo katika hafla ya kutia saini mradi wa maji ziwa Victoria kutoka kahama kwenda halmashauri ya Ushetu, ambapo amesema kuwa viongozi hawatakiwi kuwa na vikwazo katika kutekeleza na kukamilisha mradi huo utatumia miezi hadi 24 kukamilika kwake.

Kwa upande wake, waziri wa maji Juma Aweso amesema Mkandarasi anayetekeleza mradi huo akamilishe kwa wakati ili wananchi wasiendelee kuteseka kutokana na kukosa maji safi na salama kwa muda mrefu, pamoja na kuwataka viongozi ngazi ya wilaya na mkoa kuwachukulia hatua kwa wale watakaobainika kukwamisha mradi huo.

Naye, mbunge wa Jimbo la ushetu Emmanuel Cherehani katika halfa hiyo amewashukuru viongozi mbalimbali walioshiriki pamoja na kuhakikisha mchakato wa maji ya ziwa Victoria unakamilika mpaka kufikia hatua ya kutia saini.

Utekelezaji wa mradi huo, utahusisha ujenzi wa wa matanki matatu yenye ujazo wa lita 500,000, 300,000 na 100,000 katika maeneo tofauti kata ya Ulowa pamoja na bomba kuu la chuma lenye kipenyo cha kuanzia milimita 350 hadi milimita 100 lenye uwezo wa kilometa 76 kutoka katika Manispaa ya Kahama Kwenda Ulowa hadi kwenye Matanki hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *