Wakati tunasubiria remix ya ‘Dah’ sehemu ya tatu kati ya Nandy na Usher, staa huyo R&B kutoka Marekani, ameahidi kutamba jukwaa la Super Bowl, Half Time mjini Las Vegas siku ya jumapili kwenye mchezo unaowakutanisha Kansas City Chiefs na San Francisco 49ers, kuvaa viatu vyenye matairi- roller skates.
Usher amesema atafanya hivyo ilikuonesha uwezo wake wa kucheza akiwa amevaa viatu hivyo ambavyo vimekuwa maarufu tangu aliposaini mkataba wa kufanya kufanya kazi na Las Vegas (residency).
Usher atakuwa msanii wa kwanza kupanda jukwaani kama msanii huru kwenye shughuli hiyo, baada ya kuachana na lebo yake ya RCA na kutoa album – akiwa msanii huru- ijulikanayo kama Coming Home, wiki hii.