
Kufuatia matukio ya ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo yaliyojitokeza kwa vijana wa Makachu katika eneo la bustani ya Forodhani matukio ambayo yameleta athari mbaya kwa jamii na miundombinu ya Serikali Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe imetoa taarifa ya kusimamisha shughuli za Makachu.
Matukio hayo yanajumuisha upigaji wa makachu kwa kutumia mavazi yanayokwenda kinyume na utamaduni, uharibifu mkubwa Wa mifereji na miundombinu mengine pamoja na matumizi ya debe za taka kwa michezo ya vichekesho (Comedy).
Mamlaka ya Mji Mkongwe imetangaza kusimamisha shughuli za makachu hadi hapo itakapo kamilisha kuandaa utaratibu wa kuimarisha utendaji wa kazi hizo , Serikali imesema inatambua mchango wa makachu kwa kutangaza shughuli za utalii. Kwa sasa Mamlaka inaendelea na uchunguzi wa jambo hilo na wahusika watakaobainika kufanya vitendo hivyo watashughulikiwa
