Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema kuwa mpaka kufikia sasa serikali imefanikiwa kupunguza upungufu wa changamoto ya upatikanaji wa umeme kwa wastani wa megawati 218 ambapo awali ilikuwa ni megawati 421.
Kapinga ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbuge wa viti maalumu Shari Raymond aliyetaka kujua ni lini Tanesco watarekebisha tatizo la kukatika kwa umeme katika kata ya Uhuru Kusini Mkoani Kilimanjaro.
Aidha, ameongeza kuwa serikali inatekeleza mradi wa kujenga vituo vya kupoza na kusafirisha umeme katika mkoa wa Tabora ambapo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18 tatizo la kukatika umeme linalotokana na laini ndefu litaweza litakuwa limepungua.
Kuhusu suala la usambazaji wa umeme katika taasisi za elimu, afya, dini, pamoja na visima, Kapinga amesema, tayari miradi inaendelea kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini ambapo wigo wa usambazaji wa umeme huo umeongezwa kwa kilomita mbili na kufanya wigo wa sasa kuwa kilomita tatu ili taasisi nyingi ziweze kufikiwa.