Watalaam wa upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wenzao kutoka nchini Marekani wamekamilisha kambi maalum ya siku tano iliyohusisha upasuaji wa urembo na upasuaji wa matibabu (Cosmetic and Reconstructive Surgery) kwa wagonjwa nane.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kambi hiyo na kwa niaba ya timu nzima iliyoshiriki, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa MNH, Dkt. Ibrahim Mkoma, amesema upasuaji uliofanyika ni wa matibabu kwa wagonjwa waliokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo waliopata ajali ya kuungua moto na wenye misuli iliyokakamaa kutokana na majeraha n.k.

Amesema, kuna mtoto ambaye kichwa chake kilizaliwa kikiwa na vinundu vidogo vidogo mithili ya visunzua (ski…


