Kampuni ya usimamizi ya Wasanii wa muziki ya Universal Music Group (UMG), leo Feb. 1 imeziondoa nyimbo za wasanii wote wanaowasimamaia katika mtandao wa TikTok baada ya kushindwa kuafikiana juu ya mkataba mpya.
Hivyo kuanzia sasa video zote za TikTok ambazo zilitengenezwa kwa nyimbo za wasanii wanaosimamiwa na UMG hazitoweza kusikika sauti zake.
Miongoni mwa wasanii wanaosimamiwa na UMG ni pamoja na; Justine Bieber, Taylor Swift, kundi la BTS, Billie Elish, Lady Gaga na rapa Kanye West.